Joshua 22:1-4

Makabila Ya Mashariki Yarudi Nyumbani

1 aNdipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, 2 bnaye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Musa mtumishi wa Bwana aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. 3Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyowapa. 4 cSasa kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapa ng’ambo ya Yordani.
Copyright information for SwhKC